kichpox.blogspot.com
Tanzania's Leading Entertainment News,News analysis from East Africa & worldwide, multimedia interactives, opinions, documentaries, podcasts, long reads and broadcast schedule.
Feb 28, 2018
Agizo alilolitoa Waziri Mkuu akiwa mkoani Mtwara Kuhusu Watoto Wenye Ulemavu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu kutowafungia ndani na badala yake wawapeleke shule. Amesema ulemavu si kigezo cha kuwakosesha watoto hao kupata elimu na kufanya kazi, hivyo amewataka jamii kutowakatisha tamaa Alitoa agizo hilo jana (Jumanne, Februari 27, 2018) wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa majengo ya chuo cha Ualimu Kitangali,...
Maandamano yamponza Mbuge wa CHADEMA, Mkutano wake Wazuiwa2
Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare amezuiwa na Jeshi la polisi nchini kufanya mkutano wa hadhara ambao ulipangwa kufanyika leo Februari 28, 2018 jimbo Bukoba Mjini katika uwanja wa Soko la Rwamishenye. Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema wamezuia mkutano huo kutokna na hali ya usalama katika wilaya hiyo na kuhusu taarifa za watu kushawishiwa kuandamana kwenye mitandao ya jamii....
Ajirusha baharini kina kirefu Akiwa Safarini Kwenda Zanzibar
Mwanaume mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika amejirusha baharini kutoka katika boti ya Azam iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar Jumatatu, katika eneo linalohisiwa kuwa na kina kirefu.
Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii jana inaonyesha boti hiyo ikiwa imesimama eneo ambalo mwanaume huyo alijirusha huku watu wakijadiliana namna ya kumwokoa.
Tukio hilo limeelezwa kufanyika katika eneo la Bahari ya Hindi "ukishapita Msasani" ambako kuna mkondo wa maji unaodhaniwa kusababishwa na kina kirefu cha maji.
Eneo hilo lipo mwendo wa nusu saa kutoka Bandari ya Dar es Salaam, kwa boti ziendazo kasi. Safari mpaka Zanzibar huchukua saa mbili.
Video hiyo inaonyesha abiria hao wakiwa wanashangaa uamuzi wa mtu huyo kujitosa baharini huku wengine wakisikika wakisema kuwa anaonekana akiogelea.
Baadhi ya waliokuwa kwenye boti hiyo walisikika kwenye video hiyo wakiomba wapewe nafasi wajitose kwenda kumtafuta kwani wao ni mahiri kwenye uogeleaji.
"Kama vipi tumfuate, wengine tunaweza (kuogelea)... anaonekana yule, kuleee tuacheni sisi tunaoweza kuogelea tukamchukue kwasababu tunaweza jamani," alisikika mtu huyo akimwomba mmoja wa wahudumu wa boti hiyo huku akirekodi video.
Taarifa kutoka ndani ya Azam zilisema mabaharia wa boti hiyo walijitahidi kumtafuta mwanaume huyo eneo alipojitosa lakini hawakufanikiwa.

Waliojeruhiwa kwa Risasi Maandamano ya CHADEMA waachiwa kwa Dhamana
Wananchi watatu wanaodaiwa kuwa wafuasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali.
Hata hivyo, watu hao watatu wameunganishwa katika kesi ya wafuasi 28 wa CHADEMA ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyipita.
Washtakiwa hao watatu walisomewa kosa lao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita.
Wakili Mwita aliwataja washtakiwa hao watatu kuwa ni Isack Ng’aga, Erick John na Aida Olomi.
Wakili Mwita amedai washtakiwa hao, March 8, 2018 wataunganishwa na wenzao 28, ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita.
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa February 16, 2018 huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa Halali kinyume cha sheria.
Inadaiwa kuwa mkusanyiko huo ulikuwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha Taharuki kwa wananchi.
Treni ya abiria yapinduka mkoani Dodoma
Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza.
Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Othieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo wala idadi ya majeruhi.
Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya ajali.
Subscribe to:
Comments (Atom)